Washauri?
Naamini kabisa kila mtanzania anayeishi nje na anayetaka kufanya chochote nyumbani atalala usingizi mwololo akiwa na mtu au mshauri wa uhakika atakayeweza kumsaidia kwa lolote analohitaji kulifanya nyumbani!
Mimi nina washauri wangu ambao wameweza kunisaidia katika mambo mbalimbali ya kibiashara, sheria, makazi na huduma mbalimbali. Wengine nimesoma nao zamani, wengine tumekutaka katika kusafiri, kuishi sehemu moja au shughuli fulani, wengine nimekutana nao kwenye humu humu kwenye mdahalisi.
Nimewaomba washauri wangu wawe wanachangia mawazo, hoja na ujuzi walionao kwenye nafasi zao kwenye Gazeti Pepe la MtuKwao la kila mwezi, na wamelipokea ombi langu bila matatizo.
---------------------------------------------------------
Baadhi ya washauri wangu:
-Bwana Ananiah Kamundu - MD wa SisiMIZI (TZ) Ltd.
-Bwana Happy Lebe wa Halem Construction CO. Ltd.
-Bwana William Chiume wa Tanzania Investment Centre(TIC)
-Dr. Ellen Mkondya Senkoro - CEO wa Mkapa Foundation
-Bwana Kwanza Msingwana wa Toronto, Canada
-Bwana Andrew Mkapa wa Business Registration & Licensing Agency (Brela)
---------------------------------------------------------
Kama umependezeshwa na Tovuti hii basi utapenda Gazeti Pepe letu la kila mwezi litakalokuwa na mambo mbalimbali motomoto ya matukio, burudani na maoni kutoka kwa washauri.
Tafadhali, usihofu kwani sitagawa wala kuuza barua-pepe yako. Nitaitumia kukuletea Gazeti Pepe la MtuKwao

|