Home
Blog
Tovuti Zetu
Huduma
Burudani
Matukio
Biashara
TV Live
Kujitolea
Makazi
Gazeti la Mwezi
Washauri
Tanzania
Kuhusu Mimi
Tuwasiliane

[?] Subscribe To This Site

XML RSS
Add to Google
Add to My Yahoo!
Add to My MSN
Subscribe with Bloglines

 

Waraka kutoka kwa mjomba

Ndugu yangu, kila kukicha kwenye mbuga za wanyama za Serengeti, Nyumbu anapoamka tu anafahamu kwamba ni lazima aweze kukimbia zaidi ya Simba mwenye mbio kuliko wote la sivyo atakamatwa na kufanywa kitoweo. Vilevile, kila kukicha humo humo Serengeti, Simba anapoamka tu anafahamu kwamba ni lazima aweze kukimbia zaidi ya Nyumbu mwenye mbio hafifu kuliko wote la sivyo atakosa msosi na atakufa kwa njaa. Kwahiyo, haijalishi kama wewe ni Simba au ni Nyumbu, kukicha tu lazima uanze kukimbia! Kumbuka kwamba kila kitu kinawezekana ukiweza kuamini.

Ndugu yangu, dakika unazowekeza za kusoma huu waraka zinaweza kuonekana kama si kitu sana, naomba nikuambie kwamba hizi dakika ni muhimu sana kwa sababu kila dakika uliyonayo ni mwanzo wa kuzifanya ndoto zako ziwe kweli. Kutokana na dakika nzuri inakuja saa nzuri, na kutokana na saa nzuri inakuja siku nzuri halafu mwezi mzuri, halafu mwaka mzuri, mwaka huo unakufanya uwe mjenzi wa maisha mazuri, chanzo ambacho kimetokana na ile dakika nzuri ya mwanzo!

Ukiwa bado utapenda kusoma Waraka nzima bofya hapa; Waraka kutoka kwa Mjomba

Mimi?

Mimi naitwa Michael T. Mwakilasa, ni mzaliwa wa Kyela, Mbeya. Nimesoma shule za msingi za Kyela, Mwadui na Mgulani kabla ya kwenda Tambaza, Mazengo na CBE.

Hivi sasa naishi Dar-es-Salaam, Tanzania baada ya kuishi nje ya nchi kwa muda mrefu. Mwenyezi Mungu katubariki familia yetu kwa kutupa watoto wawili wa kiume Abraham na Baraka.

Familia yetu na matukio mbalimbali katika picha.

_________________________________________________________________

Tangu nikiwa mdogo nimekuwa nafanya biashara ndogo ndogo wakati huo huo nasoma, kwa muda sasa nimekuwa najifunza hii teknolojia ya intaneti na nadhani itakuwa njia mojawapo kubwa itakayotuletea watanzania maendeleo kwa upesi zaidi.

Hii tovuti nimianzisha wakati naishi Marekani ili niweze kupata habari, huduma na burudani za Tanzania sehemu moja, kwani kuna habari kwenye tovuti na blog mbalimbali za watanzania ambazo kila siku nilipenda kuzipita, nategemea wengine mtapenda mkusanyiko nilioufanya.

Baadaye nikaanza kuwaonyesha hii tovuti marafiki na ndugu zangu wakaniomba niipanue zaidi na niweze kuwakaribisha na watanzania wengine watakao pendezeshwa na mkusanyiko uliomo kwenye hii tovuti.

Kama utapenda kuanzisha tovuti, na umeupenda mfumo wangu tafadhali ingia hapa chini



________________________________________________________________ Tafadhali usisahau kijiandikisha kupata Gazeti Pepe la kila mwezi kwa kubonyeza kidude kinachosema RSS cha rangi ya machungwa pembeni kushoto kwani utakuwa unajulishwa pishi nyongeza yeyote inapotokea kwenye tovuti ya mtukwao.

Jiandikishe hapa chini, Ninaahidi sitagawa wala kuuza barua pepe yako bali nitaitumia kukuletea Gazeti Pepe la MtuKwao kila mwezi.

Gazeti Pepe
Please note that all fields followed by an asterisk must be filled in.
Barua Pepe*
Jina la Kwanza


Dar-es-Salaam