Home
Blog ya MtuKwao
Tovuti Zetu
Huduma
Burudani
Matukio
Biashara
TV Live
Kujitolea
Makazi
Gazeti la Mwezi
Washauri
Tanzania
Kuhusu Mimi
Tuwasiliane

XML RSS
What is this?
Add to My Yahoo!
Add to My MSN
Add to Google
 

Mali Asili ni urithi wetu kuufaidi!


Google
 

"Tazama ramani utaona nchi nzuri, yenye mito na mabonde mengi ya nafakaaa..." Huwa nakaa nakumbuka nilipokuwa mdogo jinsi tulivyokuwa tunaimba huu wimbo!

Tanzania inasifika sana ulimwenguni kote kwa jinsi nchi yetu ilivyo maarufu kwa mbuga zetu, mlima Kilimanjaro, mito na maziwa yenye ndege adimu dunuani, visiwa vya Zanzibar na Pemba, amani, utulivu na upole wa watanzania.

Hebu tafadhali angalia hii video:

Kama wahenga walivosema "kwenye miti hakuna wazenzi". Mimi sijawahi kwenda kwenye mbuga za wanyama, sanasana nimeona wanyama mikumi wakati nasafiri kwa basi au reli ya Tazara kwenda Kyela kuona jamaa.

Mimi naamini watanzania wengi wanaoishi Tanzania na walioko nje hawajawahi kwenda kwenye mbuga za wanyama, wengine hawaoni umuhimu wake, wengine kipato ni kidogo, wengine wangepata habari za kutosha kuhusu jinsi ya kwenda pengine wangezitembelea!wengine wanasababu mbalimbali zingine.

Kama utapenda kutembelea mbuga zetu na ungependa ufahamu gharama na vibali zake, tafadhali ingia kwenye ukurasa wa regulations and park fees kwenye hii tovuti ya Hifadhi ya Taifa;

Tanzania National Parks


footer for mbuga page