Home
Blog ya MtuKwao
Tovuti Zetu
Huduma
Burudani
Matukio
Biashara
TV Live
Kujitolea
Makazi
Gazeti la Mwezi
Washauri
Tanzania
Kuhusu Mimi
Tuwasiliane

XML RSS
What is this?
Add to My Yahoo!
Add to My MSN
Add to Google
 

Kujitolea na Maendeleo ya Mtanzania!

Kila kukicha waafrika hasa tunaoishi dunia ya kwanza tunaona kwenye luninga na kusoma kwenye magazeti jinsi waafrika tunavyozidi kuangamia kwa magonjwa, njaa, na umasikini uliokithiri.

Video ya mwaka 2000 ya ahadi kutoka kwenye nchi za dunia ya kwanza ikisomwa na aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa wakati ule Bwana Kofi Annan.

-----------------------------------------------------------------

Katika kuishi kwangu nje nimekutana na watanzania kwenye mafungu yafuatayo;

1.Wanaojihusisha kwa njia mbalimbali katika mapambano ya kutafuta suluhisho na maendeleo.

2.Wanaolaumu Serikali, Viongozi, Mifumo ya nchi na n.k

3.Wenye kuumwa na roho, lakini wamekuwa wenyeji sana wanapoishi, hawana muda wala pesa kwani madeni waliyonayo ni mengi.

4.Hawa wamekata mawasiliano kabisa na nyumbani, wanasema wao walifanikiwa kuondoka, waliobaki Afrika watajijua wenyewe.

-----------------------------------------------------------------



Bwana Hans Rosling ambaye ni daktari na mchambuzi maarufu kuhusu takwimu mbalimbali za dunia anaelezea kuhusu jinsi Afrika tunavyoweza kuondokana na umasikini.

----------------------------------------------------------------

Tafadhali ingia kwenye hii tovuti usikilize mawazo ya watu kutoka sehemu mbalimbali za dunia walikutana Arusha mwezi wa sita mwaka huu 2007. Africa: The Next Chapter

---------------------------------------------------------------

Nimepata fursa ya kuwafahamu baadhi ya watanzania na watu wa mataifa ya nje wanaojitolea kwa mali, muda na hali zao.

Nimeshuhudia wanavyojitoa nafsi zao kuacha maisha yao mazuri wanayoishi na kwenda vijijini, wanapata magonjwa, ajali na matatizo yetu mengi tu ya kiafrika lakini kila mwaka wanarudi tena!

Siena Italia kuna Bi Nancy Mwinjo na kaka yake Zoe Matei Msami, vijana wa kitanzania wanaosoma huko wamekuwa wakileta maendeleo mengi kijijini kwao Haubi na wilaya nzima ya Kondoa.

Vijana wa Muhimbili Alumni Organization (MAO), wanasidia shule yao ya msingi madawati, umeme na n.k zaidi bofya hapa.

Ujerumani kuna Dada Tausi Likokola anayesaidia watoto yatima walioachwa na wazazi wao kutokana na ugonjwa wa ukimwi. Kwa habari zao zake zaidi bofya hapa.

New York kuna vijana wa kimarekani, Edward Bergman na Robert Alsbrooks wameweza kuanzisha vituo vya elimu kwa watoto Arusha na Songea, wanapeleka madaktari wa macho na meno vijijini, kwa habari zao zaidi bofya hapa.

Je, Afrika tunahitaji pesa au ushirkiano wa kibiashara!

Kuna makampuni mengi ya misaada yanayotumia teknolojia ya mdahalisi kuweza kumuwezesha mtu yeyote na popote alipo duniani kuweza kumsaidia mtu anayeishi dunia ya tatu kwa mkopo moja kwa moja bila kupitia mlolongo wa watu wengine wa kati, zaidibofya hapa

Tafadhali angalia hii program ya PBS kuhusu Kiva.

________________________________________________________________

Kuna Shule hii inayoitwa CIDA afrika kusini, ambayo ikiigwa na nchi nyingi za afrika naamini tutapiga hatua!

________________________________________________________________

Kama Tanzania tunapata asilimia 85 ya mapato yetu ya mauzo ya nje kutokana na ukulima, na asilimia 80 ya watanzania ni wakulima, naona itakuwa jambo la busara tukiweza kuiga mfano wa Bwana Martin Burt wa Paraguaya;


kama umeiipenda hii tovuti, utapenda kutumiwa Gazeti-pepe la kila mwezi litakalokuwa na mambo motomoto yanayotokea kwenye mtukwao. Tafadhali jiandikishe hapa chini.
Gazeti Pepe
Please note that all fields followed by an asterisk must be filled in.
Barua Pepe*
Jina la Kwanza

footer for Kujitolea page