"Bongo sasa kumekucha bwana!" Joseph, aliyerejea hivi karibuni kutoka Tanzania kuona ndugu na jamaa baada ya miaka 10 anamsimulia Hamidu, mtanzania mwenzake ambaye hajarudi nyumbani tangu alipoondoka miaka 7 iliyopita.
"aah! nasikia maendeleo yapo lakini umeme wa mgao, maji shida, rushwa kama kazi, huduma za jamii bado ni mbovu" Hamidu anamjibu Joseph na kuongezea "Ajira shida kwa wasomi wanaomaliza vyuo.
Basi hawa ndugu wanazungumza kwa muda mrefu kiasi! Joseph anajaribu sana kumweleza Hamidu mambo mengi mazuri yanayofanyika nyumbani na Hamidu anamjibu Joseph kwa kumweleza mambo yasiyo mazuri anayoyasikia na anayoyasoma kwenye mitandao.
Joseph anamalizia mazungumzo yake kwa kumwambia Hamidu ana miaka miwili mpaka mitatu anarudi nyumbani kabisa. Hamidu yeye anamwambia Joseph, akipata makaratasi yake atakuwa anakwenda nyumbani kutembea na kurudi, lakini hapa ndo kafika.
Katika kuishi kwangu nchi mbalimbali, nimekutana na akina Joseph na akina Hamidu wengi tu. Mimi nadhani wote wawili wana ukweli wao katika mambo wanayoyazungumzia, ukweli ni kwamba kila mtanzania popote alipo, kama ni Marekani, Ulaya, Asia, Afrika, Uarabuni au popote duniani, ana kaJoseph au kaHamidu ndani mwake! wengine kadogo sana na wengine kakubwa sana na wengine nusunusu!
Mimi naamini watanzania wengi tuko nje ya nchi yetu kwa ajili ya kutafuta maisha mazuri ya sisi wenyewe na familia zetu. Kila mmoja wetu kafika mahali alipo kwa njia na sababu tofauti, kubaki au kurudi kunafuata njia na sababu tofauti vilevile. Mimi nadhani, popote mtu atakapoamua kuishi ni nyumbani.
Wakati tofauti huwa nakaa na kukumbuka nyumbani; vyakula, hali ya hewa, kucheza mpira, kuonana na ndugu.
Lengo la MtuKwao ni kujaribu kukusanya shughuli na maisha ya nyumbani sehemu moja, ili siku nikikumbuka nyumbani nikiasi tu kuwasha komputa na kubonyeza helufi chache na niwe nyumbani!x
_____________________________________________________________________
Jiandikishe hapa ili utumiwe Gazeti Pepe la kila mwezi litakalokuwa na mambo motomoto yanayotokea nyumbani.
Blog Blog ya Mtukwao inakuletea habari na mambo motomoto yanayotokea kwenye MtuKwao.com, Tanzania na jumuia zake dunia nzima ya mtanzania.
Tovuti Tovuti na Blog za kitanzania nyumbani na dunia kote
maliasilinaUtalii Utajiri wa Mali Asili ya nchi yetu ni urithi wetu na muhimu tuulinde, tujivunie na tuufaidi.
micheal mwakilasa Mimi naitwa Michael T. Mwakilasa, ninaamini Watanzania tukiweza kuitumia teknolojia ya intaneti kwa ufanisi mzuri itatuletea maendeleo sana.
Tuwasiliane Mawasiliano ni muhimu katika kujenga mtandao