Kutokana na takwimu za vyama vya kimataifa, uchumi wa bara la afrika unakua kwa kasi zaidi kuliko mabara mengine.
Tanzania ni nchi mojawapo katika nchi tatu zizoongoza kwa kasi ya kukua. Uchumi wa Tanzania katika miaka 10 sasa unakua kwa wastani wa 6%. Je, hali hiyo itatusaidiaje watanzania kuweza kuanzisha biashara na kuongeza ajira kwa watanzania wengi?
Ukiwa na mipango ya kufanya au bado unafanya utafiti wa biashara gani unataka kuifanya nyumbani, tafadhali unaweza kutumia tovuti zifuatazo kukusaidia zaidi;
Nimefurahishwa sana na hawa ndugu zetu wa nchi za kiafrika walioamua kutumia ubunifu, ujuzi na bidii bila kukata tamaa ya hali waliyokuwa nayo katika nchi zao na kuanzisha biashara zilizofanikiwa. Mimi naamini watanzania tunaweza kujifunza kitu fulani kutoka kwao.
Hebu mwangalia huyu mama wa kinigeria - Mama Adenike Ogunlesi alivyoanzisha nguo za watoto anazoziita Ruff 'N' Tumble.
Livingstone, Zambia - Bwana Ndaba Ndlovu alianza kama guide sasa hivi anaendesha kampuni yake ya "Touch Adventure" kwa watalii wanaopenda starehe za kukufanya damu iende mbio!
Huyu Bi Monique Maddy alikuwa na kampuni Tanzania ya simu iliyokuwa inaitwa Adesemi katika miaka ya mwishoni mwa tisini na mwanzoni mwa elfu mbili, ameandika kitabu na anaelezea kidogo kuhusu kitabu chake;
Msikilize Bwana Ali Mufuruki Mkurugenzi mkuu wa InfoTech akituwakilisha kwenye kongamano moja la kimataifa kuhusu jinsi gani ya kusaidia biashara za nchi za dunia ya tatu hasa hasa kuhusiana na fedha iliyoandaliwa na Google
Nadhani hili ni somo zuri sana kutoka kwa hawa wote wanne.