Huduma mbalimbali za kusaidia jamii
Harusi Yangu

Usafiri, Hoteli na kukodisha gari

Ununuaji wa tiketi za kusafiria unabadilika kila siku, siku hizi intaneti inakuwezesha kununua tiketi, kupata hoteli au kukodisha gari bila kwenda kwa wakala.
Kuna mshirika mmoja kaniletea tovuti yake ya kutuwezesha kupata tiketi za kwenda nyumbani kwa bei nafuu. Tafadhali bonyeza kwenye mstari uliosema International Flight Search kuingia kwenye ukurasa wa kutafuta tiketi za kimataifa.
Tafadhali Bofya hapa
Kufungua akaunti za Benki nyumbani

Miaka ya nyuma ilikuwa shughuli kubwa kufungua akaunti kwenye benki za nyumbani kwa watanzania wanaoishi nje. Kwa sasa Benki ya CRDB imerahisisha sana kufungua hizo akaunti.
Nilipofanya utafiti wangu na kuzungumza sana na Bwana Sebastian Mmasa, mimi binafsi naona kuna faida nyigi sana kwa Watanzania waishio nje kufungua akaunti nyumbani, kama ni wafanyakazi, wafanyabiashara au wanafunzi.
Kama unahitaji kufungua akaunti benki ya CRDB au una maswali, tafadhali wasiliana na wakala wa benki aliyepo kwenye nchi unayoishi au anayewakilisha ukanda wako kwa kubofya hapa
Baada ya kuzungumza sana na wakala wa Marekani, Bwana Sebastian Mmasa. Nimepata kuelewa vizuri zaidi faida na niko mbioni kufungua akaunti.
Ukiwasiliana naye atakutumia fomu yenye maswali na majibu ambayo watu wengi wanapenda kujua, fomu mbalimbali za aina za akaunti itakayokufaa, fomu ya kufanya shughuli zako za benki kwenye intaneti.
Kwa swali na mahitaji mengine wasiliana na Bwana Sebastian Mmasa:
|