"Nyumbani mbali na Nyumbani"
"Bongo sasa kumekucha bwana!" Joseph, aliyerejea hivi karibuni kutoka Tanzania kuona ndugu na jamaa baada ya miaka 10 anamsimulia Hamidu, mtanzania mwenzake ambaye hajarudi nyumbani tangu alipoondoka miaka 7 iliyopita.
"aah! nasikia maendeleo yapo lakini umeme wa mgao, maji shida, rushwa kama kazi, huduma za jamii bado ni mbovu" Hamidu anamjibu Joseph na kuongezea "Ajira shida kwa wasomi wanaomaliza vyuo.
Basi hawa ndugu wanazungumza kwa muda mrefu kiasi! Joseph anajaribu sana kumweleza Hamidu mambo mengi mazuri yanayofanyika nyumbani na Hamidu anamjibu Joseph kwa kumweleza mambo yasiyo mazuri anayoyasikia na anayoyasoma kwenye mitandao.
Joseph anamalizia mazungumzo yake kwa kumwambia Hamidu ana miaka miwili mpaka mitatu anarudi nyumbani kabisa. Hamidu yeye anamwambia Joseph, akipata makaratasi yake atakuwa anakwenda nyumbani kutembea na kurudi, lakini hapa ndo kafika.
Ipinda, Kyela
Katika kuishi kwangu nchi mbalimbali, nimekutana na akina Joseph na akina Hamidu wengi tu. Mimi nadhani wote wawili wana ukweli wao katika mambo wanayoyazungumzia, ukweli ni kwamba kila mtanzania popote alipo, kama ni Marekani, Ulaya, Asia, Afrika, Uarabuni au popote duniani, ana kaJoseph au kaHamidu ndani mwake! wengine kadogo sana na wengine kakubwa sana na wengine nusunusu!
Mimi naamini watanzania wengi tuko nje ya nchi yetu kwa ajili ya kutafuta maisha mazuri ya sisi wenyewe na familia zetu. Kila mmoja wetu kafika mahali alipo kwa njia na sababu tofauti, kubaki au kurudi kunafuata njia na sababu tofauti vilevile. Mimi nadhani, popote mtu atakapoamua kuishi ni nyumbani.
Wakati tofauti huwa nakaa na kukumbuka nyumbani; vyakula, hali ya hewa, kucheza mpira, kuonana na ndugu.
Lengo la MtuKwao ni kujaribu kukusanya shughuli na maisha ya nyumbani sehemu moja, ili siku nikikumbuka nyumbani nikiasi tu kuwasha komputa na kubonyeza helufi chache na niwe nyumbani!x
_____________________________________________________________________
Jiandikishe hapa ili utumiwe Gazeti Pepe la kila mwezi litakalokuwa na mambo motomoto yanayotokea nyumbani.
Blog ya MtuKwao Blog ya Mtukwao inakuletea habari na mambo motomoto yanayotokea kwenye MtuKwao.com, tafadhali usiache kututembelea mara kwa mara kwani tupo mbioni kufanya majambozi mengi tu!
|
Tovuti Tovuti na Blog za kitanzania nyumbani na dunia kote
|
Huduma na Shughuli za Nyumbani Ukitaka kufungua akaunti ya benki, kutafuta zawadi au bidhaa ndogondogo nyumbani
|
Burudani Hebe burudika na Musiki wa aina mbalimbali wa nyumbani na Vichekesho vya Bwana Majuto
|
Matukio Matukio mbalimbali yanayotokea nyumbani na nje yanayowahusu watanzania
|
Biashara Tanzania Je, wakati umefika wa sisi Watanzania kuanzisha biashara za kisasa
|
Tanzania Tv and Radio Live Angalia na usikilize live Tv na radio za Tanzania
|
kujitolea Kujitolea kwa aina mbalimbali kwa mtanzania na katika kupambana na matatizo ya nchi yetu na Afrika kwa ujumla.
|
Makazi, nyumba za kupanga na kununua Nyumba za kupanga au kununua, kutafuta viwanja na makazi kwa ujumla Tanzania.
|
Gazeti Pepe, Kujiandikisha Jiandikishe usikose gazeti pepe kila mwaka la MtuKwao litakalokuwa na mambo motomoto.
|
Washauri wangu wa uhakika Kuna washauri wengi wa kitanzania
|
maliasilinaUtalii Utajiri wa Mali Asili ya nchi yetu ni urithi wetu na muhimu tuulinde, tujivunie na tuufaidi.
|
micheal mwakilasa Mimi naitwa Michael T. Mwakilasa, ninaamini Watanzania tukiweza kuitumia teknolojia ya intaneti kwa ufanisi mzuri itatuletea maendeleo sana.
|
Tuwasiliane Mawasiliano ni muhimu katika kujenga mtandao
|

|